http://sk.uploads.im/t/OBNZM.jpg
Jana February 28, 2018 TCRA walitoa List ya nyimbo ambazo hazitakiwa kuchezwa katika vituo vya Redio na TV,  moja ya jambo  ambalo limekuwa gumzo ni kutoka Staa wa Bongo Fleva, Belle 9 amewashangaa (BASATA) kwa kushindwa kuwajua wasanii hata kwa majina yao.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Belle 9 amesema kitendo cha BASATA kuchanganya majina kwa kumtaja kwenye orodha ya wasanii waliofungiwa nyimbo zao ni sawa na baba kutowajua watoto zake.

“Kwahiyo mimi ni Roma Mkatoliki haya basi tongwe record baby jei mada yo yo yo Roma!  Hii ni sawa na kua na baba ambaye akisikia umekosa ana kuhukumu lakini akiulizwa jina la mwanao anaitwa nani anajiuma uma halafu analitaja jina la mtoto wa jirani ambalo huwa analiskia akiwa anakuja kukuhukumu,” -Belle 9

Last edited by SEMEDU (01-03-2018 16:06:50)