http://sk.uploads.im/t/9ZYPs.jpg
Leo March 1, 2018 Msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 14 na mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kupatikana na hatia ya kutapeli na kusababisha hasara kwa kushindwa kufika kwenye shoo.

Katika kesi hiyo iliyotolewa hukumu  imethibitika kuwa Shilole alilipwa kiasi cha Shilingi Milioni tatu na Mary Musa kwa ajili ya kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka mwaka jana 2017 katika Ukumbi wa Heineken uliopo Mbagala-Kijichi jijini Dar es Salaam lakini alishindwa kutokea kwenye shoo hiyo kama walivyokubaliana.

Kutokana na kitendo hicho,  mashabiki waliofika kwenye shoo hiyo walipandwa na hasira na kufanya fujo huku wakiharibu mali ukumbini hapo na kumsababishia mwandaaji ambae ni Mary, hasara ya Shilingi Milioni 14 ambazo mahakama imeamua Shilole azilipe kama fidia kwa mlalamikaji.