.header { background: url(images/acenavy/logo.jpg) no-repeat; height: 250px; }

mawazohuru njoo tuongee pamoja

User info

Welcome, Guest! Please login or register.


You are here » mawazohuru njoo tuongee pamoja » UJENZI » JE UNAMPANGO WA KUJENGA NYUMBA YAKO?


JE UNAMPANGO WA KUJENGA NYUMBA YAKO?

Posts 1 to 3 of 3

1

UJENZI : Unampango wa kujenga? Tazama picha 25 rangi bora za kisasa zinazopakwa ndani.
19149457_142201783017348_4461599926108678754_n

Ukuaji wa teknolojia umeongeza kwa kasi mabadiliko katika ujenzi wa nyumba zetu miaka ya nyuma wengi walipaka rangi cream au nyeupe kwa ndani tofauti na siku hizi ambapo rangi huchanganywa kwa teknolojia ya kisasa ya kutumia kompyuta na kupelekea kuongeza wigo mpana wa uchaguzi wa rangi za kupaka ndani na nje ya nyumba zetu.

Muhimu kuzingatia ni kuwa rangi hizi zinazong’aa kwasana mfano rangi ya machungwa “Orange” zinapendeza kupakwa katika ukuta mmoja tu kwa ndani na kwingine zinabaki rangi zisizo na kelele yaani zilizotulia zaidi.

kwenye vyumba vya watoto wa kiume wengi hupendelea blue wakati kwa wakike pink,purple na rangi ya machugwa “orange” au rangi ya kijani “green” hupendeza zaidi.

Utakapohitaji kununua rangi za nyumba yako ni muhimu kujua ni rangi ipi ipo katika wakati, siku hizi rangi hata gypsum zinapendeza ukiweka tofauti na nyeupe kama wengi walivyozoe

Ni muhimu kuchagua rangi kwa uangalifu. Zaidi ya kufanya nyumba yako ionekane maridadi, rangi pia inaweza kuathiri hali yako ya moyoni. Rangi nyangavu husisimua, lakini rangi ambayo si nyangavu huelekea kumtuliza mtu. Huenda rangi fulani isiangaze inapopakwa ndani ya kuta za jengo, lakini ikawa nyangavu zaidi inapopakwa nje ya jengo hilo. Fernando na Dilma wamechagua kupaka nyumba yao rangi ya manjano ya kidhahabu na “rangi nyeupe ya kijivu.” Baadaye tutaona mahali ambapo watapaka rangi hizo.

Tazama mpangilio wa rangi unaoonyeshwa hapa juu. Rangi zinazoangaliana zinaitwa rangi zenye kukamilishana, nazo huonekana ziking’aa zaidi zikiwa pamoja. Ikiwa kusudi lako si kusisimua, chagua aina mbalimbali za rangi moja.

BONYEZA HAPA KUTAZAMA PICHA 25 ZA RANGI KALI ZA KISASA KWAAJIRI YA NYUMBA YAKO

Source BLOG YA ROY24

2

:cool:  :cool:  :cool:  :cool:

3

tumeshamaliza kujenga nchi :D

Quick post

Write and submit your messageYou are here » mawazohuru njoo tuongee pamoja » UJENZI » JE UNAMPANGO WA KUJENGA NYUMBA YAKO?