.header { background: url(images/acenavy/logo.jpg) no-repeat; height: 250px; }

mawazohuru njoo tuongee pamoja

User info

Welcome, Guest! Please login or register.


You are here » mawazohuru njoo tuongee pamoja » DONDOO ZA UREMBO NA UTANASHATI » UREMBO WA NYWELE KWA KUTUMIA VITU ASILIA


UREMBO WA NYWELE KWA KUTUMIA VITU ASILIA

Posts 1 to 2 of 2

1

http://sk.uploads.im/t/t3yZ4.jpg
http://sk.uploads.im/t/aHywA.jpg

Urembo wa nywele kwa kutumia vitu asilia
Wanawake nawakumbusha kuwa si lazima kuwa mrembo utumie vitu vyenye kemikali unaweza kutumia vitu vyako nyumbani na ukaonekana mrembo zaidi.
Vitu vinavyoweza kukuza nywele zako na kuwa nzuri kama utafanyia steaming ni vingi lakini hivi hapa unaweza kutumia na vikakusaidia.
Mayai -Eggs
Mayai yana Protini nyingi hivyo ni kinga tosha ya nywele zako na kuzifanya ziwe ngumu pia huzikuza
Chukua mayai 2-3
Kwa maandalizi ya kuzifanya nywele zako zikue chukua mayai kwa idadi hiyo kisha weka kwenye bakuri yapige mpaka yachanganyike kisha paka kwenye nywele zako ambazo tayari utakuwa umeshaziosha na shampuu yako ya kawaida.
Paka mayai kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho ukifanikisha zoezi hilo kaa kwa muda wa dakika 5 kisha osha.
Bia
Kinywaji cha Bia kina vitamin B na sukari ya asili kwa ujumla vitu hivi vinasaidia kwa kiasi kikubwa kuzifanya nywele ziwe nzito na kukomaa.
Tumia bia ya Moto, ukiona umeshaosha nywele na umetumia Conditioner paka bia kwenye nywele zako kaa nayo kwa dakika kadhaa kisha osha na maji masafi.
Mayonnaise
Mayonnaise ni steaming nzuri sana kwa nywele zako cha kufanya, chukua kiasi kinachotosha paka kuanzia chini kwenye mzizi mpaka juu kisha weka mfuko ufunike nywele zako.
mayonnaise itafanya kazi kwa muda wa nusu saa kisha osha vizuri na upake mafuta yako.

Parachichi ‘Avocado’

Parachichi ‘Avocado’ ni moja ya steaming ambazo husababisha nywele kukua na huziimarisha pia mbali na kazi hiyo pia husaidia kuzilainisha kwani kazi yake ni kama ‘Conditioner’.
Husaidia kukava sehemu ambayo haina nywele hasa sehemu ya mbele ambayo nywele hukupuka.
Kuna mchanganyiko maalumu ambao husaidia kwa kiasi kikubwa kuimalisha nywele nao ni kama ifuatavyo..
½- Banana
Yai moja
Kijiko kimoja cha mafuta ya nazi
Kijiko kimoja cha mzaituni
kijiko kimoja cha asali
Changanya vyote kwa pamoja kisha weka kwenye nywele zako kaa kwa muda wa dakika 30 mpaka 45 baada ya hapo osha nywele zako kwa shampuu nzuri.

Mchanganyiko mwingine mzuri ni huu
½ kikombe cha Mayonnaise
Yai 1
Vijiko 2 vya asali
Ukishapaka mchanganyiko wako huu weka kikofia cha
plastic ili kuufanya ufanye kazi kwa haraka kaa kwa muda wa dakika 45 au 30 kisha osha utaona matokeo.

Ushauri
Nakushauri kutumia vitu hivi mara moka kila wiki kwa nia ya kujaza na kuzirefusha nywele zako ikiwa ni pamoja na kuzipa uhai wa kudumu.

2

HAYA

Quick post

Write and submit your messageYou are here » mawazohuru njoo tuongee pamoja » DONDOO ZA UREMBO NA UTANASHATI » UREMBO WA NYWELE KWA KUTUMIA VITU ASILIA