Computer ina uwezo wa kufanya mambo ambayo binadamu hatokuja kuweza kuyafanya kirahisi. Lakini, haiwezi kufanya kitu bila kupewa amri Fulani. Zaidi haiwezi kujitunza, inakutegemea wewe kwa kila kitu. Computer yako ni muhimu sana, zipo sababu nyingi za kuunga hilo mkono, umenunua kwa bei ghali (..Hata kama umenunua Used..). Programu sio pekee ni muhimu lakini ni vyema zaidi kuwa nazo kama kweli unaijali computer yako.
Kabla hata ya kwenda mbali, Tembelea Ninite , hapa utaweza kudownload program zote za muhimu bure ingawa baadhi ni kwa ajili ya kujaribu kwa muda tu na baadae itabidi ununue, usiwaze achana na zile zinazohitaji ununue zipo program nyingi sana tu za bure na bora zaidi. Tia maanani aina ya computer yako ili pindi unapo download software iweze kufanya kazi. Hapa naongelea aina kama ni 32-Bit au 64-Bit. Computer zinaweza kuwa kuwa na Operating System moja kwa mfano Windows 7, kampuni moja kwa mfano Samsung au Dell, lakini zina uwezo wa Bit tofauti, program ya 64-bit haiwezi kusoma kwenye 32-Bit, vivyo hivyo pia kwa 32-Bit. Ili kuona aina hii, Right Click (Bofya kitufe cha Kulia cha kipanya) kwenye My Computer, kisha Properties, kisha tizama sehemu iliyoandikwa System Type.

Namba #10: Google Chrome

Browser Bora duniani! Well, hii ni kwa maoni yangu na watuniaji wa mtandao wa internet pote duniani. Kati ya asilimia 80 ambazo browser kubwa zaidi zimetumika, asilimia 34.68 walitumia Google Chrome, Firefox 16.60%, Safari 16.15% na Internet Explorer 15.62%. Chrome inaload haraka zaidi kupita brower nyingine.
Ina Plugins na inaweza kucheza Video, Audio na kusoma PDF vizuri zaidi.
32-Bit: DOWNLOAD HAPA

Namba #9: Win RAR.
Hii inafanya kazi ya kufungua mafaili ambayo yako Compressed. Haya ni mafaili ambayo yamebanwa ili yawe na ukubwa mdogo zaidi unaowezekana. WinRar ni programu kwa ajili ya Windows ambayo hufanya kazi ya kuyafungua mafaili hayo na kuyatenga katika mafaili yanayojitegemea.

32-Bit: DOWNLOAD HAPA 64-Bit: DOWNLOAD HAPA

Namba #8: Adobe Reader
Njia rahisi ya kutunza mafaili na documenti nyingi hasa kwa njia ya mtandao ni katika mfumo wa PDF. Adobe Reader ndilo suluhisho bora kwa ajili ya kusoma mafaili ya aina hii.

DOWNLOAD HAPA

Namba #7: CCleaner
Super! Hii ni program nzuri sana kwa ajili ya computer yako. Inakuwezesha kusafisha computer yako na kuifanya ikae katika hali nzuri. Inasafisha cookies zote na kufanya browser zikae safi. Inafuta mafaili yote yanayobaki pindi unapo uninstall program katika registry.

DOWNLOAD HAPA

Namba #7: Internet Download Manager (IDM)
Kwa mtumiaji wa mtandao wa internet na kama una download mafaili kutoka mtandaoni. IDM ndiyo program yako. Ina download kwa kasi mara 5 zaidi ya spidi yoyote ile ya kushusha mafaili kutoka mtandaoni. Ni software ya kununua lakini usijali.
Download IDM hapa na kisha
Download Key zake hapa na utaweza kuitumia Bure Kabisa.

Namba #6: VLC Media Player
Moja kati ya program za kipekee za kufungulia mafaili ya video na muziki. VLC Media Player ina uwezo wa kucheza aina nyingi sana tofauti tofauti za mafaili ya muziki na video, pia inaweza ku convert video.
32-Bit: Download Hapa

Namba #5: AVG Antivirus
Antivirus bora ya CNET mwaka 2013. AVG imeweza kuua asilimia 80 ya virusi muda mchache tu baada ya kutengenezwa. Inaitunza computer yako kuepukana na virusi na mafaili yasiyo salama kwa computer yako.
32-Bit: Download Hapa

Namba #4: uTorrent
Hii inasaidia katika kudownload mafaili makubwa kama filamu, software mbalimbali na documenti za kushea. Utorrent hudownload mafaili ya torrent ambayo haya yame uploadiwa na watumiaji wa Utorrent. Ni mahususi kwa wapenzi wa filamu na series kwani unaweza kudownload CD/DVD nzima.
32-Bit: Download Hapa

Namba #3: Skype
Unganishwa na mtu yeyote pale duniani kupitia Skype. Unaweza kufanya mkutano na kuwasiliana na ndugu na marafiki wakiwa popote pale duniani. Unaweza kupiga simu pia ukiwa nyumbani au ofisi kwako kwenda kimataifa.
32-Bit: Download Hapa

Namba #2: Audacity
Ni programu muhimu kwa ajili ya kurekodi sauti, kuchanganya audio na kuboresha sauti na pia kubadilisha spidi ma sauti za audio.
32-Bit: Download Hapa

Namba #1: Software Informer

Ni muhimu sana ku update program zako katika PC. Pia ni vizuri kuelewa muenendo wa Drivers za computer yako. Software informer inakurahisishia kupata Driver yoyote inayohitajika katika computer yako pia inakueleza punde tu Programu Fulani inapokuwa imeboreshwa. Zaidi ya watu milioni 1 wanaitumia.
32-Bit: Download Hapa

Kwa ushauri na maoni tafaidhali usisite Kuwasiliana Nami. Nitashukuru na kufarijika sana. Unaweza pia kushea na marafiki zako kupitia mitandao ya kijamii.